Jumatano , 29th Jun , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha wakuu wa mikoa watatu pamoja na wakuu wa wilaya aliowateua hivi karibuni na kuwataka kwenda kusimamia fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Akizungumza leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, katika tukio la wakuu wa mikoa na wilaya kula kiapo cha uadilifu wa utumishi wa umma, Rais Dkt. Magufuli amewataka kwenda kusimamia haki na maendeleo na kushughulikia kero za watanzania wanaowaongoza bila kujali itikadi zao.

Rais Dkt. Magufuli amesema mara nyingi fedha za miradi zikifika kwa wakurugenzi zinashindwa kuwafikia walengwa kutokana na wakurugenzi wengi kujimilikisha fedha hizo hivyo wasimaie kikamilifu ili fedha hizo zitumike kwa miradi iliyokusidiwa.

Pia amewataka wakuu wa wilaya kuwashughulikia watu ambao pia wanahusika kuhujumu uchumi huku akitolea mfano wa mtu mmoja ambae aliekuwa anatumia mashine za EFD's kufanya miamala ya fedha kati ya milioni saba hadi nane kwa dakika.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka wakuu hao wa wilaya kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa ajili ya kuwatumikia watanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli