Jumatano , 9th Jan , 2019

Rais John Magufuli ameweka wazi kwamba amewaweka kiporo Mkuu wa Wilaya ya Gairo na Mkurugenzi wake kutokana na matendo yao ya kugombana badala ya kufanya kazi hivyo wasifikiri kwamba hafahamu.

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli

Rais Magufuli ameyasema hayo leo baada ya kumaliza kuapisha viongozi wapya aliowateua baada ya kufanya mabadiliko katika Wizara mbalimbali pamoja na Makatibu wa Wizara.

Rais amesema kwamba anafahamu changamoto ni nyingi katika utendaji wa kazi ingawa yapo mengine mazuri wanayofanya na kuwataka wahakikishe wanajitoa kwa maslahi ya wananchi.

"Nafahamu hizi kazi zina changamoto nyingi sana mfano kuna DC Gairo na Mbunge hawaelewani mpaka Mbunge anapost kumtukana DC tena mke wa mtu, hajui kama anaweza upoteza Ubunge, 'i hope' siku moja ataomba msamaha kwenye Bunge", amesema Mh Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameongeza kwamba, "halmashauri ya Nyasa wanagombana sana Dc na Mkurugenzi, nimewaangalia tu! nimewaachia kiporo chao. Pale Dodoma Mkurugenzi wa Jiji na DC walikuwa wanagombana nika-send meseji nikawaambia endeleeni kugombana siku moja mtagombania Vijijini, wamenyamaza naona yameisha".