Rais Magufuli
Katika ziara hiyo, Rais Magufuli pamoja na mambo mengine alipozungumza na wananchi wa eneo hilo ametangaza kuahirisha mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2020 hadi hapo tishio la kuenea kwa virusi vya Corona litakapomalizika.
Amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kufikiria kwa kina na kupata ushauri wa wasaidizi wake na kwamba pesa zote zilizopangwa kwa ajili ya kukimbiza mwenge zipelekwe katika Wizara ya Afya kwaajili ya maandalizi ya wagonjwa watakaopatikana na Corona.
"Kwa mamlaka niliyonayo, Mwenge wa mwaka huu hautakimbizwa mpaka hili swala la ugonjwa wa Corona litakapoisha. Zile hela zilizokuwa zimepangwa kwaajili ya kukimbiza mwenge zipelekwe Wizara ya Afya kwaajili ya maandalizi ya wagonjwa watakaopatikana na Corona, kwa hiyo waliokuwa wamezoea kulia kwenye mwenge walie tu", amesema Rais Magufuli.
Aidha katika suala la ujenzi wa barabara za juu (Ubungo Interchange), Rais Magufuli ameelezwa kuwa ujenzi umefikia asilimia 70, huku ukitarajiwa kukamilika kwa gharama ya shilingi Bilioni 230.






