Marais watano wa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Jakaya Kikwete wa Tanzania na mwenyeji wa mkutano Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Katika mkutano huo Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania anatarajiwa kukabidhiwa Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, wadhifa ambao alikuwa akabidhiwe mwezi Desemba mwaka jana, lakini hakuweza kuhudhuria mkutano huo kutokana na kwenda kutibiwa nchini Marekani.
Marais wote watano wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Jakaya Kikwete wa Tanzania na mwenyeji wa mkutano Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Mbali na masuala ya uhusiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii miongoni mwa mataifa hayo, kujadiliwa katika kikao hicho, pia maombi ya nchi za Sudan Kusini na Somalia kuomba uanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki yatajadiliwa.