Amiri jeshi mkuu Rais Jakaya Kikwete ametoa nishani kwa askari 59 wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania wakiwemo askari wastaafu waliyofariki dunia na waliopo kazini wakiongozwa na mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Katika tukio hilo limefanyika kwenye chuo cha maafisa wa jeshi Monduli Rais Kikwete alianza kwa kuwavisha nishani mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na mnadhimu mkuu wa jeshi Luteni Jenerali Samweli Ndomba.
Wakizungumza baada ya kutunukiwa nishani hizo zikiwemo nishani za operasheni safisha Msumbiji na nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania askari wastaafu akiwemo brigedia jenerali Hasani Ngwilizi amesema askari wastaafu wamefarijika kuona jeshi bado linawajali na waliopo kazini wamesema nishani hizo zimewaongezea ari ya kutekeleza majukumu yao katika jeshi huku wawakilishi wa askari waliofariki dunia wakiitaka serikali iendelee na utamaduni wa kuzikumbuka familia za watu waliotoa mchango mkubwa kwa taifa.
Tukio hilo pia lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Rais mstaafu wa awamu ya pili mzee Alli Hasani Mwinyi waziri mkuu Mizengo Pinda mawaziri wakuu wastafu Edward Lowasa na mzee John Malechela pamoja na mawaziri wa serikali ya awamu ya Nne.