Alhamisi , 23rd Jun , 2016

Rais wa Rwanda Paul Kagame anatarajiwa kufanya ziara nchini Tanzania julai Mosi mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine, atafungua maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara Jijini Dar es Salaam,(DITF),Sabasaba.

Rais wa Rwanda Paul Kagame(Kulia) Akiongea Glasi na Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustin Mahiga, amesema ziara hiyo ni mwendelezo wa uhusiano mzuri baina ya nchi hizo.

Dkt. Mahiga amesema kuwa rais Magufuli amemualika Rais Kagame kuja nchini kunatokana na ziara yake aliyoifanya nchini Rwanda ambapo pamoja na mambo mengine walikubaliana kushirikiana kwenye Nyanja mbalimbali.

Moja kati ya mambo waliyokubaliana ni pamoja na wataalamu wa nchi hizo mbili kukaa pamoja na kujadiliana kwa kina mambo mbalimbali katika kuleta maendeleo ya taifa moja na nyingine katika nyanja tofauti.