Jumatatu , 20th Sep , 2021

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amepongezwa kwenye mitandao ya jamii kwa kusafiri na idadi ndogo ya maofisa kuhudhuria Mkutano wa Mkuu wa 76 wa Baraza la Umoja wa Mataifa Jijini New York.

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema

Rais Hichilema amesafiri kwenda kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa kwa kutumia ndege ya shirika la ndege la Qatar akitokea uwanja wa ndege wa Lusaka akiambatana na mawaziri wawili tu.

Rais Hichilema ambaya amekuwa akisisitiza matumizi mazuri ya rasilimali za nchi, amesafiri na Waziri wa Mambo ya Nje Stanley Kakubo na Waziri wa Fedha Dk. Situmbeko Musokotwane.

Kwa kitendo hicho Rais Hichilema amepongezwa mitandaoni kwa kubana matumzi ya serikali huku wakitolewa mifano ya mataifa ya Zimbabwe na Malawi kwa kusafiri maafisa wengi safari za nje