Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi Salum Msangi.
Akithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao katika matukio tofauti Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi Salum Msangi amewataja watuhumiwa hao ambao watafukishwa mahakamani kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria ni Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi Salum Msangi raia wa Ufaransa ambaye aliwajeruhi watu sita na Artur Miarka ambaye alikutwa na bunduki na risasi aina ya Shotgun.
Aidha Kamishna Msangi ametoa wiki moja kwa wageni wakiwemo wawekezaji na wazalendo ambao wanamiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha kabla ya jeshi hilo kuanza oparesheni maalum ya kuzisaka silaha kutokana na kuwepo kwa ongezeko la watu kuwa na silaha Zanzibar.
Hili ni tukio la Nne katika kipindi kifupi kwa jeshi la polisi kufanikiwa kuwakamata watu wenye silaha na wengine kukutwa na mabomu kisiwani Zanzibar hali ambayo wananchi wengi wakihoji hali ya usalama na vipi silaha hizo zinapita bila ya kugundulika.