Jumatano , 19th Jul , 2023

Rais wa Urusi hatahudhuria mkutano wa kilele nchini Afrika Kusini mwezi ujao, kwa mujibu wa rais wa Afrika Kusini  Cyril Ramaphosa.

Tangazo hilo linakuja baada ya kiongozi wa Afrika Kusini kusema jaribio lolote la kumkamata Vladimir Putin litakuwa tangazo la vita dhidi ya Urusi.

 

Kama Putin angeondoka katika ardhi ya Urusi, angekuwa chini ya waranti wa kukamatwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).Afrika Kusini ni nchi iliyotia saini mkataba wa ICC na inatarajiwa kusaidia katika kukamatwa kwa Putin.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov ataiwakilisha nchi hiyo katika mkutano huo wa siku mbili badala yake, kwa mujibu wa rais wa Afrika Kusini.Katika taarifa yake, ilielezea makubaliano ya Putin kutohudhuria kama ya makubaliano  na kusema yamekuja kufuatia  idadi ya mashauriano juu ya mkutano huo.

Wafuasi wa Urusi wamekosoa uamuzi huo wakisema Afrika Kusini inapaswa kusisitiza na kutumia uhuru wake kumlinda na kumtetea rafiki yake.

  Mkusanyiko wa nchi za Brics - kifupi cha Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini  mnamo Agosti unaonekana na wengine kama mbadala wa kundi la G7 la uchumi wa juu.