Alhamisi , 29th Sep , 2022

Takribani watu 19 wamepoteza maisha baada ya kunywa pombe inayosemekana kuwa na sumu huko nchini Morroco. 

 Tukio hilo limejiri kwenye duka moja lililopo katika jiji la kaskazini mwa nchi hiyo la  Ksar el-Kebir.

Makumi ya watu wengine wamepelekwa hosptali wakiwa kwenye hali mbaya huku wawili kati yao wakiwa kwenye chumba cha uangalizi maalum cha ICU. 

Mtu Mmoja mwenye umri wa miaka 48 amekamatwa akihusishwa na tukio hilo. Polisi wamesema kwamba wamekuta lita nyingine 50 za pombe hiyo kwenye hifadhi yake.   

Kuuza pombe kwa waumini wa dini ya kiislamu ni marufuku nchini  Morocco, lakini imekua ikiuzwa kwenye migahawa mbalimbali nchini humo. 

Mwezi wa nane mwaka huu watu 8 walipoteza maisha baada ya kunywa pombe iliyokua na sumu huko kaskazini mwa mkoa Oriental nchini humo, mwaka jana takribani watu 20 walipoteza maisha mwezi Julai kwa matukio kama hayo katika maeneo ya Oujda mashariki mwa Morocco.