Taarifa kutoka kwa Katibu Mwenezi wa Chama hicho, Ado Shaibu amesema kwamba polisi wanawalazimisha watu kutawanyika katika ukumbi huo.
Leo, Viongozi waandamizi wa ACT Wazalendo wakiongozwa na Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe, Makamo wa Kwanza wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif, Naibu Kiongozi wa Chama, Duni Haji walikuwa wakitarajia kukutana na wanachama wa ACT - Wazalendo.
Viongozi wengine ambao wanatarajiwa kuwa kwenye mkutano huo ni pamoja na Mwenyekiti wa chama Ndugu Yeremia Maganja, Makamo Mwenyekiti Bara Ndugu Shaaban Mambo, Katibu Mkuu, Dorothy Semu na Naibu Katibu Mkuu, Msafiri Mtemelwa pamoja na viongozi wengine wa kitaifa na wa mkoa wa Dar es salaam.
Taarifa zaidi zitaendelea kukujia endelea kufatilia www.eatv.tv





