Jumatano , 25th Jun , 2014

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salam nchini Tanzania limekamata pikipiki 668 zinazotiliwa mashaka na kuzikagua, na zile ambazo zitabainika kutumika katika ujambazi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Mkuu wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, kamishna wa polisi Suleiman Kova.

Akizungumza jijini Dar es salaam Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es salaam Kamishna Suleimani Kova, amesema msako huo pia utahusisha kuwasaka wale wote waliohusika na tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi Mtawa wa kanisa katoliki Sista Cresincia Kapuri.

Aidha Kova amewataka wafanyabishara na taasisi wasitumie njia ya mkato kwa faida ya ulinzi wa maisha na mali zao na badala yake watumie usafirishaji wa fedha kwa njia salama ikiwemo za mitandao ya simu na cheki.