
Mawe ya madini ya dhahabu yenye uzito wa gramu 6753 .4 ambayo thamani yake ni Sh Bilioni 9.2 yamekamatwa na Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga yakitoroshwa kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga na Carboni yenye mchanga unaodhaniwa kuwa wa dhahabu ambao unauzito wa kilogramu 261.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amesema mawe ya madini yamekamatwa yakitoroshwa kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kupitia msako na doria uliofanyika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga.
Katika hatua nyingine Kamanda Magomi amesema wizi wa mafuta ya Diesel kwenye mradi wa Reli ya kisasa SGR umekuwa ukifanywa na baadhi ya wafanyakazi kwa kushirikiana na watu wa nje ambapo wamebuni mbinu ya kuweka kwenye chupa za plastiki za lita moja na nusu.
Amesema kupitia msako uliofanywa na Jeshi la polisi wamekamata lita 603 za mafuta ya Diesel yanayotumika kwenye mradi wa Reli ya kisasa SGR katika maeneo unapoendelea ujenzi huo ambapo changamoto ya wizi wa mafuta ilikuwa imepungua lakini kwa sasa wezi wa mafuta wanashirikiana na wafanyakazi wa mradi huo kwa kutumia bunduki aina ya Riffle yenye namba 2/49pf78701ambayo ilikuwa inatumika katika shughuli za ulinzi bila kibhujumu serikali.
Amesema pia wamekamata buali,ikiwa ni pamoja na kukamata madawa ya kulevya aina ya bangi yenye uzito wa kilo gramu 71 na pakiti 120 za vipodozi vinavyoaminika kuwa na sumu.