Jumanne , 12th Dec , 2023

Wafanyabiashara wakubwa wilayani Songwe wametakiwa kuwachukua Askari Polisi kwa ajili ya kuwasindikiza (Escort) wanapokuwa kwenye shughuli zao za kwenda kuuza madini na kuchukua hela na kuzipeleka benki ili kuepuka kufanyiwa uhalifu wanapokuwa njiani.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe ACP Theopista Mallya

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe ACP Theopista Mallya ameyasema hayo leo Desemba 12, 2023, alifungua mafunzo ya ulengaji wa shabaha kwa wamiliki wa silaha za kiraia wilaya ya Songwe na kusema kuwa, ni vyema unapokuwa unaenda kupima dhahabu au unapokuwa na hela nyingi ni bora kuchukua askari kwa usalama wako na mali yako.

"Unakuta mtu anaenda kupima dhahabu au kupeleka hela benki bila ulinzi kutokana na hivyo anavamiwa na kuchukuliwa hela pamoja na mali zake, mara nyingine na yeye anapoteza uhai kwa jambo ambalo angefuata utaratibu wa kuchukua Askari Polisi kwa ajili ya ulinzi madhara hayo yasingeweza kutokea," amesema Kamanda Mallya.

Kwa upande wa wafanyabiashara hao walimuahadi Kamanda Mallya kutekeleza agizo hilo ili kuwa salama wao na mali zao.