Taarifa ya jeshi hilo imeeleza kuwa, dereva wa basi hilo amekamatwa kwa ajili ya mahojiano zaidi na kwamba mara baada ya uchunguzi kukamilika na akipatikana na kosa hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Ajali hiyo imetokea mara baada ya basi hilo lililokuwa likitoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam, kumgonga mwendesha pikipiki aliyejulikana kwa jina la Babu Isaya na kusababisha kifo chake papo hapo.
Aidha majeruhi watatu wa ajali hiyo waliendelea na safari mara baada ya kupata matibabu.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure, kwa ajili ya uchunguzi na utakapokamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.