Jumanne , 12th Jul , 2016

Watu wawili wanaosadikika kuwa ni majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi, wakati wa majibizano ya kurushiana risasi na polisi walipokuwa kwenye jaribio la uporaji katika eneo la Kigugu, kata ya Makandana wilayani Rungwe, Mkoani Mbeya.

Tukio hilo limetokea, majira ya saa kumi jioni katika eneo la Kigugu, kata ya Makandana Wilayani humo wakati Majambazi hao wakiwa na wenzao wawili walipojaribu kumvamia mfanyabiashara GADI MWAINUNU (56) kwa nia ya kufanya kitendo cha uporaji.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya ZAHIRI KIDAVASHARI amesema kuwa jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa kuna kundi la majambazi watano waliokuwa wamejipanga kufanya uhalifu kwenye taasisi mojawapo ya kifedha na kwa wafanyabiashara wa Mjini Tukuyu.

KIDAVASHARI amesema majambazi hao wakiwa na pikipiki mbili zisizokuwa na namba za usajili walifika nyumbani kwa mfanyabiashara Gadi MWAINUNU mkazi wa Kagugu kwa lengo la kufanya uhalifu ambapo hata hivyo walikabiliana na askari polisi ambao walikuwa tayari wamejianga na kufanikiwa kuwauwa wawili huku wengine wawili wakikimbia baada ya kujeruhiwa.

Msikilize hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Zahiri Kidavashari
Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Zahiri Kidavashari