Jumatano , 14th Jan , 2015

Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma linawashikilia wanafunzi 84 wa chuo kikuu cha dodoma UDOM kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani chuoni hapo.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa chini ya ulinzi

Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma linawashikilia wanafunzi 84 wa chuo kikuu cha dodoma UDOM kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani chuoni hapo na kufanya maandamano haramu kuelekea katika ofisi mbalimbali za viongozi wa umma zilizopo mjini dodoma.     
    
Taarifa ya kukamatwa kwa wanafunzi hao inatolewa na kamanda wa polisi mkoa wa dodoma kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi David Misime ambapo ameeleza kuwa wanaoshikiliwa ni wanafunzi wa programu maalum ya diploma ya ualimu.

Kamanda Misime amesema chanzo chya uhalifu huo ni kikao walichofanya wanafunzi hao mnamo tarehe 13 January mwaka huu wakidai kuongezewa posho ya chakula.

Hata hivyo kwa upande wa uongozi wa chuo hicho ukizungumzia madai hayo umesema kuwa wenye mamlaka ya kuzungumzia swala la kuongezewa posho ni bodi ya mikopo na siyo chuo huku ukiwataka kufuata taratibu za kuwasilisha madai yao.