Jumanne , 16th Dec , 2014

Mkoa wa Arusha umeungana na mkoa wa Dar es Salaam katika kampeni za kukabiliana madereva walevi na wanaopiga na kupokea simu wakiwa wanaendesha magari tatizo ambalo limekuwa miongoni mwa vyanzo vya ajali za barabarani zisizo za lazima.

Wakizungumza katika uzinduzi wa kampeni hizo jijini Arusha mratibu msaidizi kikosi cha usalama barabarani mkoani Arusha Bw, Emilian Kamhanda pamoja na kushukuru kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu.

Mkuu wa kampuni ya Vodacom Kanda ya Kaskazini wa Bw, Henry Tzamburukaz, amesema wataendelea kutoa ushirikiano wa kukabiliana na majanga yanayoepukika likiwemo la ajali za barabarani.

Katika uzinduzi huo wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom wameshirikiana na askari wa usalama barabarani na wajumbe wa baraza la taifa la usalama barabani kuhamasisha na madereva juu ya suala hilo na kuwagawia pete maalum za kuwatahadharisha kutotuma ujumbe wa simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.