Jumapili , 29th Jun , 2014

Wajumbe wa muungano wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA ndani ya Bunge Maalumu la Katiba, wameombwa kurejea katika bunge hilo ili kuendelea na mchakato wa kujadili rasimu ya pili ya katiba.

Waziri mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda.

Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema hayo bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha bunge la bajeti huku vikao vya bunge maalumu la katiba vikitarajiwa kuanza mwezi Agosti.

Kwa mujibu wa waziri mkuu Pinda njia pekee ya kumaliza kasoro kama zinavyoelezwa na wajumbe kutoka UKAWA ni kwa kukaa mezani na kuzirekebisha badala ya kususia mchakato mzima.