Piere akiwa na Waziri Mkuu.
Amemhakikishia hilo wakati akizungumza naye katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, ambapo Piere alikwenda kutembelea kwa mwaliko wa Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Hayo yanajiri ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kutoa kauli ya kukosoa tabia ya watu kuvipa muitikio mkubwa vitu visivyo na msingi, akitolea mfano Mchekeshaji huyo aliyejizolea umaarufu kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.
Katika hafla iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ambayo ilikuwa na malengo ya kutokomeza ziro katika wilaya hiyo, Makonda alisema kwamba watu wa 'hovyo' kama Pierre hawapaswi kupewa nafasi kwenye vyombo vya habari, hali iliyozua gumzo kubwa.
Miongoni mwa kauli hizo, Makonda alisema,"Wakina mama kama hawa wanaojituma na kuhangaika kwa ajili ya watoto, wao ndio tuwape kipaumbele, sio hawa walevi walevi, yaani unakuwa na taifa ambalo watu wa hovyo ndio wanakuwa maarufu”.




