
Mfanyabiashara kutoka jijini Dar es Salaam aliyejulikana kwa jina la Sudi Nyumbi, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na pembe hizo alizokamatwa nazo katika kijiji cha Kitandiuka akiwa njiani kuzisafirisha mahali kusipojulikana.
Akisimulia tukio lilivyotokea, afisa wanyamapori wilaya ya Kilombero Madaraka Amani amesema askari wanyamapori waliokuwa kwenye doria walimuona mfanyabiashara huyo akiwa na mtu mwingine wakiwa na pembe hizo za tembo na kwamba mara walipobaini kuwa wanafuatiliwa waliamua kukimbi na kutelekeza mzigo ambao kwa wakati huo walikuwa wameupakia kwenye baiskeli.