Alhamisi , 29th Aug , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji nchini, wamezindua mpango wa kutokomeza wahamiaji haramu mkoani humo alioupa jina la ''Pekenyua Tukufukunyue''.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda (kushoto) na Kamishina msaidizi wa uhamiaji mkoa wa DSM Edmund Mroso.

Mpango mkakati huo umezinduliwa leo Agosti 29, na kuwataka viongozi wote wa mitaa kuhakikisha wanaweka mifumo rasmi itakayomtambulisha mwananchi wa eneo lake, jambo litakalosaidia kuondoa uhalifu pamoja na wananchi kutoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa mtu wanayemtilia mashaka.

''Wahamihaji haramu nchini ni jambo la hatari kiusalama kwakuwa baadhi yao wanafanya uhalifu wa Wizi, Ubakaji, Uporaji, wanatumia rasilimali za nchi, wanatumia fursa ambazo zilipaswa kuwanufaisha wazawa ikiwemo Afya, Elimu na Ajira, kusababisha msogamano wa watu magerezani pamoja na kuwa Chanzo cha Migogoro'' amesema RC Makonda.

Kutokana na hilo Makonda ameviagiza vyombo vyote vya ulinzi na usalama, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Viongozi wa Kata na Mitaa kuhakikisha Mpango huo unafanikiwa kwa 100%.