Jumanne , 13th Aug , 2019

Mkuu wa Mkoa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema kuwa uchumi wa mwananchi wa Kagera umekua ukilinganisha na miaka iliyopita kutoka kiasi cha shilingi 667,000 mwaka 2010, hadi kufikia shilingi 1300,000 mwaka 2018.

Hayo ameyabainisha wakati akizungumza na wafanyabishara pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi ya Tanzania katika mataifa ya Kenya, Rwanda, Burundi na DR Congo katika kongamano la wiki ya uwekezaji mkoani humo.

"Mwaka 2010 pato la mwananchi wa Kagera lilikuwa takribani Tsh, 667,000, toka mwaka 2018 kwa takwimu zilizopo pato la mwananchi wa Kagera ni Tsh, 1300, 000 lakini pato jumla la mkoa limepanda toka Tsh, 1.3 trilioni mwaka 2010,  mpaka Tsh, 4.9 trilioni  mwaka 2018", amesema  RC Gaguti.

Aidha RC Gaguti ameongeza kuwa Kagera ni mkoa wa 24 kati ya mikoa 26, ambao unachangia asilimia 3.6% katika pato la Taifa.