Jumapili , 26th Aug , 2018

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, ameomba msamaha kwa watoto waliofanyiwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji kingono na Makasisi wa kanisa hilo na kueleza nia yake ya kuona haki inatendeka dhidi ya waathirika wa vitendo hivyo.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.

Papa Francis ameomba msamaha huo leo Agosti 26, huko Knock nchini Jamhuri ya Ireland wakati wa siku yake ya pili ya ziara yake ya kihistoria nchini humo. Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na Papa nchini humo baada ya miaka 39

Papa Francis, amewaambia maelfu ya waumini waliojitokeza kumsikiliza kwamba, vidonda vya maumivu vilivyotokana na Makasisi wa Kanisa hilo viko wazi ni changamoto kwa kanisa kusimama imara katika kuhakikisha ukweli na haki inapatikana.

Hatua hii inakuja baada ya waendesha mashtaka nchini Marekani kubaini kuwa zaidi ya watoto 1,000 huko jimbo la Pennsylvania walifanyiwa ukatili huo.