
Akiongea katika hafla iliyoandaliwa Ikulu ya Nairobi katika siku yake ya kwanza katika ziara yake papa Francis amemtaka pia Rais Kenyatta kulinda maliasili ambazo Kenya imkebarikiwa na Mungu.
Aidha, Papa Francis ameitaka serikali ya Kenya kujenga utamaduni wa kuvumiliana na majadiliano katika kutatua mifarakano ili kudumisha misingi ya amani.
Kwa upande wake Rais Kenyatta amemuomba Papa Francis amuombee Mungu ili aweze kuiongoza Kenya kwa kufuata usawa na kukabiliana na vitendo vya rushwa.