Balozi Shabat ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, katika maadhimisho yanayofanyika kila mwaka yajulikayo kama DAY OF QUDS kwa ajili ya kuwakumbuka wapalestina wanyonge sambamba na kuikumbusha dunia kupambana na unyanyasaji unaoendelea nchini hiyo.
Balozi Shabat amesema, inashangaza kuona dunia inakaa kimya, vyama vya kutetea haki za binadamu vikishindwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu ambao kwa kiasi kikubwa unagharimu maisha ya wapalestina kwa muda mrefu sasa.
Naye Balozi wa Irani nchini Tanzania Mhe. Mehdi Jafari ameiomba Tanzania kuisaidia Palestina kuondokana na kadhia hiyo kama ambavyo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alivyoiunga mkono taifa hilo kutokana na uonevu dhidi ya mataifa kandamizi.
Maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wapalestina nchini Tanzania na Mkurugenzi wa Kitivo cha Mwalimu Nyerere Prof. Issa Shivji.

