Jumatatu , 11th Oct , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewaonya wakuu wa mikoa na viongozi wengine wa serikali kutokuwa miungu watu kwenye maeneo yao ya kazi badala yake wakashirikine na wananchi kusukuma maendeleo ya taifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ametoa onyo hilo leo Oktoba 11, 2021 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma, wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua, ambapo amesema hatokuwa na ustahimilivu kwa viongozi wa aina hiyo kwani amekuwa akirudia mara kadhaa jambo hilo.

''Hili nalirudia na leo nalisema tena sitegemei wakuu wa mikoa kuwaona mnakuwa miungu watu kwenye maeneo yenu, mko kule kuwatumikia watu sio watu kuwatumikia nyie, sitawavumilia,'' amesema Rais Samia Suluhu.

Kwa upande mwingine Rais Samia amewaonya wakuu wa mikoa na kuwataka kujiweka kando na vitendo vya rushwa.

“Sitegemei wala sitastahamili kumuona Mkuu wa Mkoa anaingia kwenye vitendo vya rushwa, nyie ndio wa kusimamia sheria hivyo mkafanye hivyo,” ameongeza Rais Samia.

Tazama Video hapo chini akiongea zaidi