Ijumaa , 16th Oct , 2015

Serikali imeahidi kuifanya mikoa ya Nyanda za Juu kusini kuwa kitovu cha uzalishaji maziwa kwani ina mazingira mazuri yanayofaa kwa uzalishaji na ufugaji wa Ng'ombe wa Maziwa.

Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi , Dkt.Titus Kamani

Akiwa katika ziara ya kutembelea wadau wakubwa wa sekta hiyo mkoani Iringa hivi karibuni waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi Dkt. Titus Kamani amesema azma hiyo itafanikiwa kupita mpango wa maboresho ya sekta ya mifugo.

Amesema pia azma hiyo itafanikiwa kupitia mradi wa uendelezaji wa sekta hiyo ya maziwa Afrika Mashariki (EADD) unaotekelezwa katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.

Kwa upande wake meneja wa mradi wa EADD 2 Tanzania, Mark TSOXO amesema nchini Tanzania mradi huo unatekelezwa katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe.