Ijumaa , 25th Mar , 2016

Biashara ya kitoweo na nyama za kuchinja imeendelea kama kawaida katika masoko na maduka ya kuuzia nyama jijini Dar es Salaam, licha ya imani ya dini ya Kikristo kuweka zuio la ulaji wa nyama ya damu katika siku ya leo ya Ijumaa Kuu.

Kuku wa Kienyeji

Hali hiyo imebainika leo hii wakati EATV ilipotembelea maduka hayo ambapo katika soko maarufu kwa biashara ya kuku wa kienyeji la Kawe jijini Dar es Salaam, walaji wameshauriwa kununua mapema kitoweo hicho kutokana na uwezekano wa kuadimika siku ya Jumapili ambapo ndio kilele cha sikukuu ya Pasaka.

Bw. Vicent Charles Malamba ni mfanyabiashara wa nyama ya ng'ombe ambapo yeye amelalamikia hali mbaya ya kiuchumi inayowakabili Watanzania wengi kuwa imekuwa ikisababisha idadi ndogo ya wateja wanaokwenda kununua vyama katika maduka yao.

Kwa upande wao, baadhi ya wateja wa nyama wamewashauri wenzao kupenda kununua vyakula vya asili na kuepuka vile vilivyolimwa au kuzalishwa kwa kutumia madawa kutokana na uwezekano wa kuwa na madhara ya kiafya.