Alhamisi , 22nd Jun , 2023

Mwanamke mmoja nchini Kenya amejifungua wakati akiwa kwenye treni ya Madaraka Express iliyokuwa ikielekea Mombasa 

Kwa Mujibu wa mtandao wa Twitter wa shirika la reli la Kenya, mwanamke huyo alimkaribisha mtoto wake kwa usaidizi wa daktari ambaye alikuwa ndani ya usafiri huo na mhudumu wa abiria.

"Tulibarikiwa kuwa na Dkt. Indanyenyi Luseso ambaye alitoa huduma hiyo, akisaidiwa na Mhudumu wetu wa Abiria, Bi. Mary Nyiha" Shirika la Reli la Kenya liliandika pamoja na picha zinazoonyesha mhudumu akiwa amemshika mtoto.

Mwanamke huyo baadaye alikimbizwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Mariakani kwa usaidizi zaidi wa kimatibabu