Kushoto ni Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo, na kulia ni Kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe.
Nondo ametoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, mara baada ya yeye kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo hilo ambalo lilikuwa likiongozwa na Kiongozi Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe.
"Mji wa Kigoma mjini kwa muda mrefu umekuwa nyuma kiuchumi na shughuli za mzunguko wa kifedha na hilo ni jambo ambalo zitto alilipigania na ni miradi mingi alikuwa amekwishaianzisha, hivyo na mimi nitakuwa na uwezo wa kuendeleza yale ambayo aliyaanza na kuongeza yale ambayo alikuwa hajayaanza, na yale ambayo kwa miaka mitano hakuyafanya basi sisi wengine tutayafanya kama chama kitatupa ridhaa" amesema Abdul Nondo.
Tazama video hapa chini.







