Jumanne , 18th Apr , 2023

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Musoma Vijijini na baadaye jimbo la Butiama kuanzia 2000 hadi 2020 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nimrod Mkono, amefariki dunia.

Nimrod Mkono, enzi za uhai wake

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mtoto wa Nimrod Mkono, aitwaye Abbas Mkono, amesema kifo cha baba yake kimetokea leo Aprili 18, 2023.

Mbunge huyo wa zamani alizaliwa Agosti 18, 1943 katika Kijijini cha Busegwe, Kata ya Busegwe, wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Imeelezwa kwamba katika jimbo la Musoma Vijijini na baadaye Butiama, Nimrod Mkono alijenga shule za msingi na sekondari ikiwemo Chifu Ihunyo, Chifu Wazangi, Oswald Mang’ombe, shule ya sekondari Butuguri na shule ya sekondari Kasoma.

Aidha wakati wa uhai wake alishirikiana na serikali katika kufanikisha kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere.

Mungu aipumzishe kwa amani Roho ya Mzee Nimrod Mkono.