Jumatatu , 12th Mei , 2014

Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini Tanzania NIMR leo imetangaza kuanza mara moja kwa utafiti wa ugonjwa wa homa ya Dengue katika jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine nane ya hapa nchini.

Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini Tanzania, NIMR, Dkt Mwele Malecela.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa NIMR Dk. Mwele Malecela amesema kwa Dar es Salaam utafiti huo utachukua muda wa mwezi mmoja na utahusisha wilaya zote za jiji ambazo
ni Ilala, Kinondoni, na Temeke.

Takwimu za ugonjwa wa Dengue kwa nchi nzima zinaonyesha kuwa kuna jumla ya wagonjwa 400 ambao wamethibitika kuugua ugonjwa huo hadi sasa,na umeshasababisha vifo vya watu watatu, ambapo idadi ya wagonjwa waliolazwa hivi sasa Dar es Salaam ni 60 kati ya hao 42 wanatoka Kinondoni, 14 Temeke, na 4 wanatokea Ilala.