Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba,
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba, kwa meneja wa wakala hiyo kanda ya kusini katika ziara yake ya kukagua na kuongea na watumishi wa ghala la Taifa la Hifadhi ya Chakula.
Dkt. Tizeba amesema kuwa takribani kila kijiji na kata kunakuwa na ghala la kuhifadhia chakula hivyo hawana budi kwenda moja kwa moja kwa wahusika kununua mazao hayo ili kutoa tija kwa wakulima.
Aidha Waziri huyo ametoa Onyo kwa watumishi wa wakala huyo kutoanzisha vituo vyovyote kwa ajili ya manunuzi na atakaebainika kufanya hivyo basi hatua kali zitachukuliwa juu yake.