Uzinduzi wa nembo ya Bank ya Posta (TPB).
Kufuatia hali hiyo, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC ) imeiagiza benki hiyo kupeleka mikataba miwili ya zabuni ya utengenezaji wa nembo ya benki kwa ajili ya kupitia baada ya kubaini upungufu.
Akizungumza jana Agosti 21, 2019 Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naghejwa Kaboyoka, amesema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha mashirika yanafuata sheria ya manunuzi ya umma ili kufanya kazi kwa ufanisi na kuongeza mpato ya Serikali kuu.
''Wanashindwa kutimiza na kusimamia fedha za umma wakijua kuwa watabebwa bebwa tu, wanapaswa kutambua Serikali haitaingilia hilo'' amesema Mwenyekiti wa PAC.
Ripoti ya CAG ilibainisha kuwa, utengenezwaji wa nembo ya benki hiyo uligharimu kiasi cha shilingi milioni 495, ambapo CAG alisema uamuzi wa bodi ya wazabuni ni wa kutia shaka kwani gharama hiyo ilikuwa na ongezeko la mara mbili ya zabuni ya kwanza iliyokuwa imepitishwa.