Jumatatu , 21st Aug , 2023

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemteua Nelly Msuya kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA).

Kushoto ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Nelly Msuya

Pamoja na uteuzi huo, ameunda timu ya wataalamu kutoka sekta ya maji watakaofanyia kazi changamoto ya huduma ya maji kwa wakazi wa jiji la Mwanza sambamba na kusimamia kukamilika kwa mradi wa kuongeza maji katika mfumo wa usambazaji maji Jijini humo.

Timu hiyo itaongozwa na wataalamu kutoka Wizara ya Maji makao makuu ambao ni; Mhandisi Mkama Bwire, na Mkurugenzi wa Usambazaji Maji, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)  na Mhandisi Charles Mafie, Mkurugenzi Msaidizi Uendeshaji na Matengenezo, Wizara ya Maji.

Aidha, timu hiyo itahusisha, Mhandisi Nikas Mugisha, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma.
Mhandisi Anthony Mayunga, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora.
Mhandisi Valentine Njau, Meneja wa Miradi ya Majisafi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)
Mhandisi Mwandamizi Ishmael Kakwezi, Mtaalamu wa Usimamizi wa Miradi.