Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima amesema hayo mara baada ya kikao na watendaji wa tume kabla ya uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika jumamosi ijayo (Februari 17).
Mkurugenzi huyo amesema kuwa tume imejipanga kuanza kutoa vipindi vya elimu ya mpiga kura mfululizo hadi siku ya uchaguzi, elimu ambayo itakua ikigusia mada mbalimbali za uchaguzi ikiwemo haki na wajibu wa mpiga kura, wakala wa vyama vya siasa na msimamizi wa uchanguzi.
Msikilize hapa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima akitolea ufafanuzi baadhi ya mambo.







