Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva ametangaza majimbo mapya ya uchaguzi 26, huku Jiji la Dar es Salaam yakiongezeka majimbo mawili ya Mbagala na Kibamba.
Tume imetangaza majimbo hayo kwa mujibu wa Ibara ya 75(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina jukumu la kuchunguza mgawanyo wa Jamhuri ya Muungano katika Majimbo ya Uchaguzi.
Akitangaza majimbo hayo leo Jijini Dar es Salaam Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema miongoni mwao majimbo 20 yameanzishwa kwa kigezo cha ongezeko la halmashauri na majimbo 6 yameongezeka kwa kigezo cha idadi ya watu.
Kwa ongezeko hilo la majimbo 26 kwa Tanzania Bara linaongeza majimbo ya Uchaguzi kuwa jumla ya Majimbo 265 huku visiwani Zanzibar yakifikia majimbo 54 kutoka 50 ya awali..
Orodha ya majimbo mapya yote iko hapa:-
MAJIMBO YALIYOANZISHWA KWA KIGEZO CHA ONGEZEKO LA HALMASHAURI
Majimbo 20 yanayoanzishwa kutokana na kuanzishwa kwa
Halmashauri mpya ni:
1. Handeni Mjini
2. Nanyamba
3. Makambako
4. Butiama
5. Tarime Mjini
6. Tunduma
7. Nsimbo
8. Kavuu
9. Geita Mjini
10. Mafinga Mjini
11. Kahama Mjini
12. Ushetu
13. Nzega Mjini
14. Kondoa Mjini
15. Newala Mjini
16. Mbulu Mjini
17. Bunda Mjini
18. Ndanda
19. Madaba
20 Mbinga Mjini
MAJIMBO YALIYOANZISHWA KWA KIGEZO CHA IDADI YA WATU
Majimbo 6 yanayoanzishwa kutokana na idadi ya watu ni:
1. Mbagala – Dar es salaam
2. kibamba – Dar es salaam
3. Vwawa – Mbeya
4. Manonga - Tabora
5. Mlimba - Morogoro
6. Ulyankulu - Tabora
Fungua kiambatanisho