Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Said Miraji, akizungumza katika moja ya mikutano yao.
Akizungumza katika Mkutano maalum wa chama cha ADC leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama hicho Said Miraji Abdallah amesema kuwa kuna watu wenye sifa ambao wanakosa haki yao ya msingi wakiwemo wafungwa, wagonjwa, na watanzania walio nje ya nchi ambao wanashindwa kupata haki yako kutoka na mfumo wa sasa wa uandikishaji.
Bw. Miraji ameongeza kuwa kuna watu ambao wanaweza kuachiwa magerezani wakati zoezi la uandikishaji limeshapita hivyo litawafanya washindwe kushiriki katika uchaguzi mkuu hivyo tume haina budi kuziangalia sheria zake upya.
Wakati huo hou Aliyekuwa mbunge wa Wawi Zanzibar kupitia Chama cha WanancHi (CUF) Hamad Rashid amejiunga rasmi na chama chake kipya cha ADC leo na kukabidhiwa kadi namba moja.
Akiongea na waandishi wa habari Hamad Rashid ametumia fursa hiyo kutangaza nia ya kuwania urais wa Zanzibar ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwa tiketi ya chama hicho.