
Picha ya Mabwawa.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni Kongwa leo Septemba 27, Ndugai amesema wilaya hiyo ina maji mengi ya mvua ambayo yatasaidia kwenye kilimo cha kiangazi.
"Tunalo ombi maalumu, wilaya hii ya Kongwa tuna maji mengi sana ya mvua yanayopita, tukipata mabwawa kama manne hivi makubwa suala la kilimo cha kiangazi litakuwa ni katika sehemu kubwa sana ya uchumi wa eneo hili” alisema Job Ndugai
Aidha Ndugai aliendelea kuwasihi wanakongwa kujitokeza siku ya kupiga kura kwa ajili ya Chama cha Mapinduzi, katika ngazi zote nchini.
“Lakini cha muhimu ni kile kichinjio chetu 28/10 kupiga kura kwa Chama cha Mapinduzi si Kongwa tu, mkoa mzima na nchi nzima"alisema Job Ndugai