Euphomia Edward, Mratibu Mtandao wa kutokomeza ndoa za utotoni nchini.
Mratibu wa mtandao huo Euphomia Edward amesema hayo leo jijini, Dar es salaam, wakati alipokuwa akizungumza na EATV ikiwa ni katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani tarehe 11 mwezi huu.
“Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 36 ya watoto wa kike wamefunga ndoa wakiwa na umri mdogo jambo linalokatisha ndoto zao hasa za kupata elimu huku wengine wakishindwa kuhitimu hata shule za msingi”amesema Euphomia
Amesema kwa sasa wao kwa kushirikiana na serikali wamejikita zaidi kuhakikisha elimu inafika si tu kwa jamii bali pia kwa mtoto wa kike mwenyewe kufahamu haki zake za msingi ili kukomesha ukatili huo kwa watoto wa kike.