Alhamisi , 20th Jul , 2023

Ndege ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yenye usajili namba JW 9127 iliyokuwa imebeba marubani wawili imepata ajali na kutumbukia ziwani wakati ikijaribu kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Bukoba leo Julai 20, 2023.

Ndege ya JWTZ iliyoanguka ziwani leo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera ACP Blasius Chatanda amesema kuwa ajali hiyo imetokea wakati marubani hao walipokuwa wanafanya majaribio angani ya kurusha ndege na kwamba chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na kwamba hakuna kifo kilichotokea.

Ikumbukwe Novemba 6 mwaka jana, ndege Precision Air ilitumbukia ziwani na kusababisha vifo vya watu 19 na kuokolewa 24 baada ya marubani kushindwa kuona njia ya kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba kutokana na hali mbaya ya hewa.