Serikali ya Ujerumani imeipatia Tanzania msaada wa ndege mbili za doria kwa ajili ya kukabiliana na ujangili wawanyamapori wakiwemo tembo katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba.
Akizungumza jijini Arusha mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) bw. Alan Kijazi amesema ndege hizo zenye thamani ya dola laki tano zinatarajiwa kuwasili nchini na zitasaidia kupambana na ujangili.
Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya wanayapori Tanzania Bw Martin Loiboki amesema licha ya kasi ya ujangili kuendelea kupungua changamoto bado ni kubwa.
"Wakati mnajipanga kukabiliana nao wanajipanga kutengeneza mbinu mpya ya kufanikisha kufanya uhalifu lakini unapopata changamoto unapata akili mpya ya kukabiliana nayo" alisema Loiboki.
Msaada huo ni sehemu ya matokeo ya ziara ya Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Dk. Frank Walter aliyoifanya nchini na kukutana na wadau mbalimbali mkoani Arusha wakiwemo wa sekta ya uhifadhi.