Jumatano , 28th Oct , 2015

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro NCAA, imetoa shilingi 2.4 bilioni kwa mwaka huu wa fedha kwa baraza la wafugaji wa Ngorongoro ili kuwezesha miradi ya kusaidia jamii inayoishi ndani ya mamlaka hiyo.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Ngorongoro, Salustin Hallu

Akizungumza na waandishi wa habari jana afisa utalii na utamaduni wa baraza la wafugaji Oludupo Olonyoke amesema tayari fedha hizo zimeanza kutumika katika kulipia ada wanafunzi 903 kujenga zahanati na nyumba za walimu.

Amesema pia baraza hilo limeanzisha vitega uchumi ndani ya hifadhi na kwa sasa linakamilisha ujenzi wa jengo la makazi ya muda ili kuweza kusimamia vitega uchumi huo kwa ukaribu zaidi.

Awali afisa maendeleo ya jamii wa Ngorongoro, Salustin Hallu amesema NCAA kupitia miradi yake ya ujirani mwema imetoa msaada mbalimbali kwa jamii inayozunguka hifadhi hiyo.