Jumatano , 13th Apr , 2022

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imeombwa kutoa bei mpya ya nauli, za mabasi ya mikoani na daladala ili kuwawezesha kuendesha biashara zao katika kipindi hiki ambacho gharama za maisha zimeingezeka tofauti na awali.

Wamiliki wa makampuni ya mabasi wamebainisha kuwa nauli zinazotumika sasa zilikokotolewa mwaka 2013, na kwa sasa nauli hizo haziendani na gharama za uendeshaji, huku wamiliki wa daladala nao wakilaumu kuhusu faini nyingi na kubwa zinazowakabili, ambapo wameomba ongezeko la shilingi mia nne kwenye nauli za daladala.

Kwa upande wake Mtedaji Mkuu wa LATRA Gilliad Ngewe  amebainisha kuwa baada ya kupokea maoni kutoka kwa wadao hao, mchakato wa kupata nauli mpya zitakazotumika kwenye daladala na Mabasi ya mikoani.

Katika kuangazia mapokeo ya watumiaji wa usafiri huo, kuhusu ombi la kupanda kwa nauli, Mwenyekiti wa Chama cha kutetea haki za Abiria bwana Hassan Mchanjama ameshauri nauli hizo ziendelee kubaki kama zilivyo, na badala yake wamiliki watumie njia nyingine kama ukataji wa tiketi mtandaoni ili kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara zao.