.jpg?itok=MuTlBz1B×tamp=1486743582)
Waziri Nape Nnauye
Kupitia ukurasa wake wa twitter, Waziri Nape amepongeza hatua hiyo na kusema kuwa hiyo itakuwa ni hatua muhimu katika kuratibu vita hiyo dhidi ya dawa za kulevya, iliyotangazwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
"Uteuzi huu wa Mhe. Rais una ujumbe mkubwa sana kwenye vita dhidi ya Madawa ya kulevya! Hasa proper Coordination ya Vita hii tukufu!" Ameandika Nape.
Rais Magufuli, leo tarehe 10 Februari, 2017 amemteua Bw. Rogers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (Drug Control and enforcement Authority) ambaye atasaidiwa na Bw. Mihayo Msikhela ambaye anakuwa Kamishna wa Operesheni na Bw. Fredrick Kibuta ambaye anakuwa Kamishna wa Intelijensia.
Ikumbukwe kuwa siku chache baada ya Paul Makonda kutaja majina ya wasanii wanaodaiwa kuhusika na dawa hizo akiwemo Muigizaji Wema Sepetu, Waziri Nape kama waziri mwenye dhamana na wasanii alitoa maoni yake, na kushauri kuwa busara ilipaswa kutumika kataja majina ya wahusika, kwa madai kuwa ni hatua inayoweza kuchafua taswira za baadhi ya watu kwenye jamii, endapo watakutwa hawana hatia.
Ushauri huo wa Nape, baada ya siku chache uliokuja kuonekana ni kama vile unapingwa na Rais Magufuli alipotoa amri ya kukamatwa kwa mtu yoyote anayehusika na dawa hizo bila kujali umaarufu.
Ujumbe aliouweka leo Nape, unaweza kutafsiriwa kuwa ni njia ya kukazia ushauri wake, kuwa suala la dawa za kulevya linapaswa kushughulikiwa kisheria na kiutaratibu badala ya kutaja majina ya watu bila uratibu maalum.
Sikiliza hapa ushauri uliotolewa na Nape, siku ya Jumapili iliyopita baada ya Makonda kutaja majina ya wasanii