Jumapili , 2nd Aug , 2015

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa CCM jimbo la Segerea anayemaliza muda wake

Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangaza rasmi kujiunga na CHADEMA

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa CCM jimbo la Segerea anayemaliza muda wake, Dkt. Milton Makongoro Mahanga ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).baada ya kutotendewa haki katika mchakato wa kura za maoni hapo jana.

Dkt. Mahanga ametangaza uamuzi huo leo mbele ya waandishi wa habari akiwa nyumbani kwake Segerea mwisho, ambapo amesema ameamua kuachana na Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na (CHADEMA) baada ya kushuhudia mbinu chafu zilizotumia na baadhi ya wagombea dhidi yake.

Aidha Dkt. Makongoro amesema sababu nyingine ni pamoja na kupingwa na viongozi wa chama chake na kuongeza kuwa kama Chadema itampokea anaamini atakuwa sehemu salama katika harakati zake za kisiasa.