Jumanne , 8th Apr , 2014

Naibu waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika nchini Tanzania Mh Godfrey Zambi amepinga utozaji wa bima ya moto kwa wakulima wanaomiliki mashamba yenye hati za kimila yenye ukubwa wa zaidi ya hekta 10 katika wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.

Mh. Zambi amefikia hatua hiyo baada ya aina hiyo mpya ya kodi kuja na viwango vikubwa, ambavyo pia vimekuja kipindi ambacho kiuchumi wakulima wengi hawawezi kuimudu kwa kuwa bado mavuno hayajaanza.

Kwa upande wao wakulima katika wilaya hiyo ya Mbozi wamependekeza serikali kuachana na bima ya moto na badala yake kuelekeza bima hizo kwenye mashamba ya kahawa, hasa kwenye majanga ya asili kama mvua za mawe, ambazo zimekuwa zikiwatia hasara wakulima kwa baadhi ya misimu.