Ijumaa , 10th Nov , 2023

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amewaahidi wananchi akifika kaburini kwa Hayati Magufuli ataongea nae na kumwambia mema yanayoendelea kufanywa na mrithi wake Dk. Samia Suluhu Hassan

Amesema mengi yaliyoachwa yanaendelea ikiwa ni pamoja na mikopo ya wanafunzi wa elimu wa juu, huduma za maji, nishati na miundombinu ya barabara.

Makonda ameyasema hayo akiwa njiani kuelekea Chato kuzuru kaburi la Hayati Dk. John Pombe Magufuli ambapo amesema amepata malalamiko ya wananchi kuhusi vitendo hivyo na yeye akiwa ni msaidizi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan hawezi kuacha wananchi kuonewa na baadhi ya watendaji wasio waaminifu na kudhulumu haki za wanyonge.

Katika hatua nyingine Makonda amewaagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Tanzania TAKUKURU kuchunguza viashiria vya Rushwa katika Wilaya ya Muleba mara baada yakusema kuna viashiria vya harufu ya rushwa katika eneo hilo.