Ijumaa , 24th Mar , 2023

Mwanaume mmoja mwenye umri zaidi ya miaka 50 aliyejulikana kwa jina la Hakimu Juma, mkazi wa  Chamwenda kata ya Nyansaka wilayani Ilemela jijini Mwanza amejikuta matatani baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka saba mtoto wa jirani yake.

Inadaiwa kwamba mzee  huyo amekuwa na tabia ya kuwashika makalio pamoja na sehemu za siri mabinti wa mtaa huo hadi alipofikia hatua ya kumuingilia kimwili binti huyo wa miaka saba anayesoma darasa la pili

Mama mzazi wa binti aliyebakwa aaaakaeleza namna alivyogundua tukio hilo la binti yake kuingiliwa na baba huyo.

‘nilikuwa namwambia sasa wewe unaumwa hujasema umepatwa na nini, sasa nikawa  namuangalia nikaona suruali aliyokuwa amevaa ipo magotini na chupi pia imevuliwa nikamgeuza wakati namgeuza nikaona michirizi kalowa nikauliza wewe umepata UTI niliponusa mashuka nikasikia harufu ya maji ya kiume"

Kufuatia tukio hilo EATV ikazungumza na balozi wa serikali ya mtaa huo wa Chamwenda Hassan Ngiziki na kusema mara baada ya mtuhumiwa huyo kufanya tukio hilo walibaini kuwa amekuwa na tabia ya kushika makalio na sehemu za siri baadhi ya mabinti wa mtaa huo ndipo akawasiliana na vyombo vya dola na kumkabidhi kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria